Category Archives: CCT Programs

CCT YAFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

 Leo ni siku ya saba(7) ndani ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. CCT kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wametoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya msingi Ilolo na kwa  wazazi wa eneo hilo.  Mratibu wa Mradi wa mwanamke Jasiri(CCT) Mkoa wa Dodoma , Dada Elizabeth Ngede ametoa ufafanuzi wa kazi zinazotekelezwa na CCT ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia. Naye Afisa maendeleo H/Wilaya Mpwapwa Dada Sky Thomas amesisitiza wazazi

Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili-Kijiji cha Kiziwa kata ya Kiroka Mkoani Morogoro.

Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zinaendelea katika mikoa yote, ambapo leo CCT kwa kushirikiana na shirika la TCRS wametoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kijiji cha Kiziwa kata ya Kiroka Mkoani Morogoro. Eneo hili linakabiliwa na vitendo vya ubakaji hasa kwa watoto wadogo wengi wao wakiwa wanafunzi.Washiriki wameweza kueleza vitendo vya ukatili vinavyotesa jamii yao. Mzee Mchalichaly Msemaji wa TUPO Kiziwa Group amesema vyombo vya sheria vumekuwa vikipata changamoto ya kutoa maamuzi

KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI JUU YA USAWA KWA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI

Kongamano la Viongozi wa dini mbalimbali linalowahusisha TEC,CCT &BAKWATA juu ya usawakatika huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma za Bima ya afya, ulipaji kodi, elimu, uchumi n.k Baadhi ya wajumbe wakiongoza mjadala wa nini kifanyike kuhakikisha watu wote wanapata huduma kwa usawa, hususani kulinganisha huduma za kijamii kwa walioko vijijini na mjini Kongamano hili limehudhuliwa na wawakilishi wa makatibu wakuu wa TEC,CCT &BAKWATA Dr. Camillius D.N Kassala TEC  Bi. Clotilda Ndezi CCT Shk Mohamed Khamis Said BAKWATA Baadhi ya washiriki

UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

MABADILIKO YANAANZA NA MIMI Kuanzia tarehe 25 Novemba, siku ya kwanza ya kampeni ya Kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto ambapo uzinduzi wake umefanyika katika ukumbu wa Julius Nyerere International Convention Centre Dar es Salaam. Kampeni ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni wakati wa kutafakari juu ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo. Huu ni wakati wa kutafakari, kupaza sauti na kuelimisha jamii kuhusu vitendo

CCT conducted a workshop with Danmission at CCT Office in Dodoma to develop a new Proposal (2021) for the project of Interfaith Relations

On 16th to 19th November 2020 CCT conducted a workshop with Danmission at CCT Office in Dodoma  to develop a new Proposal (2021) for the project of Interfaith Relations to University Students in five Universities, UDOM, Mipango, Mzumbe, Sua and SAUTI Mtwara. The goal of the Project is to empower youth engage in peace and Development in Tanzania Bellow are Pictures for the members in the workshop

Jukwaa la wajane na Wagane wa Kikristo Tanzania limefanyika leo Tarehe 6 Novemba 2020 Dodoma.

Jukwaa la wajane na Wagane wa Kikristo Tanzania limefanyika leo Tarehe 6 Novemba 2020 katika ukumbi wa KKKT Kanisa kuu Dodoma. Dhima kuu ikiwa ni Kuhakikisha wanawake na watoto wanajengewa uwezo wa kiroho, kielimu na kiuchumi ili waweze kuzimudu changamoto na kustawi kimaisha na kumtumikia MUNGU Mgeni Rasmi Ask Boniphace Msufa alizindua kipindi cha sauti ya ushindi ambacho kitakuwa kinarushwa hewani kupitia Redio ikiwa ni jitihada za kuwajengea uwezo wanawake wajane kiroho na kiuchumi.

Tathmini ya mradi wa Mwanamke Jasiri (Mid Term Evaluation)

Watafiti kutoka kampuni ya Mais Professionals’ Consultants-MPC wakiwa katika zoezi la tathmini ya kati kwa kazi zilizofanywa na mradi wa mwanamke Jasiri. Tathmini hii inafanyika  kwa vikundi vinavyonufaika na mradi huu katika mikoa minne (Mara, Dodoma,Mbeya,Songwe na Mbeya). Mradi wa mwanamke jasiri unasimamiwa na  Jumuiya ya kikristo Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD).

WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WALIOGOOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI MKUU – 2020 KATIKA MKOA WA SONGWE

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (C.C.T) kupitia Mradi wa Mwanamke Jasiri kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) iliandaa Warsha ya Wanawake kutoka katika vikundi vya Wanawake Wajasiriamali kutoka katika Halmashauri za Wilaya Mbozi, Ileje, Momba pamoja Halmashauri ya Mji wa Tunduma waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Mkoani Songwe. Warsha ilifanyika katika ukumbi wa Kal (Kal Hall) uliopo Vwawa Wilayani Mbozi. MALENGO YA WARSHA Malengo ya Warsha yalikuwa yafuatayo:- Kuwaelimisha juu ya

« Older Entries