CCT YAFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA


 Leo ni siku ya saba(7) ndani ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. CCT kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wametoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya msingi Ilolo na kwa  wazazi wa eneo hilo. 


Mratibu wa Mradi wa mwanamke Jasiri(CCT) Mkoa wa Dodoma , Dada Elizabeth Ngede ametoa ufafanuzi wa kazi zinazotekelezwa na CCT ikiwemo kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia.

Naye Afisa maendeleo H/Wilaya Mpwapwa Dada Sky Thomas amesisitiza wazazi kuwa na lugha nzuri kwa watoto kwani watoto hujifunza kutokana na yale wazazi wanayoyafanya. Pia ameshukuru sana CCT kwa umoja ambao umekuwa ukifanyika katika harakati za kuisadia jamii katika kujikwamua kimaisha.


Vitendo vya ukatili wa kijinsia havikubaliki na tumekuwa tukivipinga hapa shuleni kila wakati ili kuwalinda wanafunzi wetu. Baadhi ya wazazi huwaita watoto majina mabaya kitu ambacho kinawafanya watoto kujiona hawana thamani yoyote. Hayo ameyasema Mwalimu Neema Sanga ambaye ni mlezi wa wasichana katika shule hiyo.


Kikundi cha ngoma cha Ahadi ilolo, mashairi kutoka kwa wanafunzi na mlemavu wa macho toka kikundi cha Walemavu Dada Lusia nao wameburudisha kongamano hilo huku wakitoa ujumbe wa kupinga vitendo vya ukatili kwa njia hiyo.


Viongozi mbalimbali akiwemo mtendaji wa kata,  wenyeviti wa vijiji jiranii, waratibu wa mradi ngazi ya jamii na wasaidizi wa kisheria na wadau wengine wameshiriki kongamano hilo na kutoa michango mbalimbali ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Leave a Reply