CCT yazindua mradi wa kilimo cha umwagiliaji Kongwa

Tarehe 11 /10/209 Jumuiya ya Kikrito Tanzania (CCT) ilizindua mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa wanavikundi vya pamoja katika kijiji cha Laikala wilayani Kongwa.

Mradi huu umehusisha uchimbaji wa kisima kinachoweza kuzalisha maji lita elfu kumi na nane kwa saa, kuweka pump kwa ajili ya kupeleka maji kwenye eneo la umwagiliaji umbali wa kilometa moja na nusu na kuweka miundo mbinu ya umwagiliaji. Eneo la umwagiliaji lina ukubwa wa ekari arobaini. Ambapo wanavikundi wa Pamoja wanategemea kulima mboga mboga na mahindi n.k. Mradi huu utawezesha uwepo wa usalama wa chakula na utunzaji wa mazingira. Mradi huu umetekelezwa kwa pamoja na Shirika la Tearfund na kukabidhiwa rasmi kwa dayosisi ya Mpwapwa Anglikana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa katika kuendeleza na kusimamia pamoja na wanavikundi.

Leave a Reply