Viongozi wa Dini mbalimbali Mkoa wa Dodoma wametoa elimu kwa njia ya redio (Dodoma FM) namna ya kuendelea kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya CORONA. Elimu hiyo imehusisha sana namna ambavyo wanajamii wanashauriwa kuzingatia katika kupunguza au kutokomeza kabisa maambukizi ya virusi hivyo. Wamehimiza waumini kuendelea kuchukua taratibu zote zinazotolewa na wataalamu wa Afya pamoja na kuendele kumwomba mwenyezi Mungu. Elimu hiyo imeratibiwa na CCT kupitia Idara y Afya Makao makuu Dodoma
Afisa kilimo,mifugo,uvuvi na ujasiriamali wa CCT kupitia mradi wa lishe endelevu, Sembael Mfangavo akitoa elimu kwa vitendo namna ya kutengeneza chakula cha ziada(uji wa lishe) kwa watoto kuanzia umri wa miezi sita na kwa kina mama wajawazito na wanaonyonyesha. Mafunzo haya yamefanyika katika kikundi cha Tupendane kilichopo kata ya kikuyu kaskazini mtaa wa mission wilaya ya Dodoma jiji. Aidha ikiwa lishe ni swala mtambuka Afisa huyo amepata wasaa wa kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima wa mbogamboga namna ya kutambua wadudu na magonjwa shambulizi na njia sahihi ya kukabiliana nayo katika bustani za mbogamboga wanazolima ikiwa ni sehemu ya upatikanaji wa mlo kamili. Kikundi hiki kinasimamiwa na CCT kupitia mradi wa lishe endelevu unaofadhiliwa na USAID. Tupendane ni kikundi ambacho kimeshatembelewa na Katibu Mkuu wa CCT Mchg.Canon Dkt.Moses Matonya kuona shughuli wanazotekeleza. Lishe Endelevu imekuwa ikitoa elimu ya lishe kwa jamii hasa kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, vijana erika balehe na wanaume ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa watoto walio katika umri chini ya miaka miwili na upungufu wa damu kwa kina mama wajawazito. Jamii inafundishwa kujikita katika uzalishaji na ulaji wa mazao ya mbogamboga kwa lengo la uimarisha afya. Kupitia mradi huu CCT imeweza kufikisha elimu hiyo kwa wilaya nne za mkoa wa Dodoma zikiwa ni Dodoma jiji,Halmashauri ya Bahi,Kondoa TC&DC
CCT yashiriki Mkutano ulioandaliwa na Wizara ya afya na viongozi wengine wa dini juu ya utekelezaji wa dawa kinga(PrEP) ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI. Picha ya pamoja kati ya watumishi wa CCT na Naibu Waziri wa Afya, Katibu mkuu wizara ya Afya na Mganga Mkuu Mkoa wa Dar es salaam na viongozi wengine
CCT kupitia mradi wa Lishe endelevu wameshiriki kwenye maadhimisho ya mbio za Mwenge ambao unapokelewa leo tar28/07/2021 katika viwanja vya shule ya Msingi Ipagala Dodoma. Lengo la mradi ni kuelimisha jamii juu ya lishe bora hasa kwa wanawake walio katika umri wa kujifungua na wenye watoto chini ya miaka miwili ili kuondokana na udumavu.
Familia ya Mchungaji Canon Moses Matonya wamefanikiwa kutoa msaada kwa kaya 63 Kijiji cha Ikowa Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma kwa kuwaunganisha na Bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa (iCHF). Kaya 63 kila moja ikiwa na wanufaika 6 na jumla ya wanufaika 378 wameunganishwa na Mpango huu ili kuwawezesha huduma za matibabu.