More details

Elimu ya kujikinga na magonjwa hatari ya mlipuko

Elimu ya kujikinga na magonjwa hatari ya mlipuko ikiwemo Ebola na Uviko 19. Hapa ni viongozi toka Makanisa ya Kikristo ndani ya Studio za Clouds FM wakieleza namna ambavyo jamii inapaswa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Ebola ambao upo nchi jirani ya Uganda. Viongozi hao wamesisitiza jamii kuendelea kuhamasika katika kupokea chanjo ya Uviko 19 ambayo imeleta matokeo chanya katika jamii zetu na ulimwengu kwa ujumla