IBADA ILIYOANDALIWA NA CCT YA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUTUFIKISHA MWAKA 2021

Leo tarehe 8/1/2021 CCT Makao makuu Dodoma tumefanya ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kutuvusha salama mwaka 2020 na kutufikisha salama mwaka 2021. Tuliongozwa na Zaburi 136:1-4,23-26. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele……….”Ibada hii imeongozwa na mchg David Kalinga na mnenaji wa neno akiwa Mchg Modest Pesha. Ibada iliambatanishwa na Ibada ya ushirika Mtakatifu na kutoa sadaka ya shukurani ikiwa ni pamoja na kutoa vitu mbalimbali kama nguo, viatu nk. Sadaka hiyo itaelekezwa kwa wahitaji.

Leave a Reply