Donate

Umuhimu wa CCT Day || Ask. Dkt. Alinikisa Cheyo

CCT Day ni kwa ajili ya kuelimishana juu ya Umuhimu wa CCT, Kujua chimbuko lake, Wanachama , kazi za CCT na Malengo ya baadae ya CCT, na namna gani ya kukiendesha chombo hiki ikiwa ni pamoja na sadaka toka makanisa wanachama ambazo zinapatikana hasa katika hiyo siku ya Maadhimisho. Maadhimisho haya yanafanyika Juma la Mwisho la Mwezi wa Tano, ambapo mwaka huu kilele ni Tarehe 30 mwezi mei.

Maandalizi ya CCT DAY|| Mchg:Canon David Mdabuko Mwenyekiti CCT Dodoma JIJI

Viongozi wa CCT Mkoa wa Mwanza wakiwatakia wakrito wote heri ya maandalizi ya CCT DAY

Maandalizi ya CCT DAY || SERENGETI

OMBIL LA KUCHANGIA UJENZI WA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA CCT DODOMA

Jumuiya ya Kikristo Tanzania kupitia Mkutano Mkuu wa 29 uliofanyika Julai 2017, pamoja na mambo mengine ulipitisha Mkakati wa miaka mitano wa CCT kujitegemea kiuchumi.  Mojawapo ya mapendekezo ya kimkakati ni kuandaa na kufanya uchangiaji wa njia ya Harambee.  Kwa msingi huo, Mkutano wa Halmashauru Kuu ya 52 iliyokutana tarehe 12-13/7/2018 Dodoma ilipitisha andiko kuhusu Harambee ya Kitaifaambayo ilifanyika Julai 2019. 

Zoezi la Kuchangia juu ya Kitega uchumi hiki bado linaendelea, Hivyo wewe kama mdau/Rafiki unaombwa kutoa mchango wa kuchangia kiasi chochote ulichonacho.

Unaweza kuchangia kupitia  njia zifuatazo

Bank:

Jina la Akaunti: CCT Jengo

Namba za Akaunti CRDB Account No. 0150281796400

Asanteni sana na Mungu awabariki .

Mchg. Can. Moses Matonya

KATIBU MKUU