Fundraise

OMBIL LA KUCHANGIA UJENZI WA JENGO LA KITEGAUCHUMI LA CCT DODOMA

Jumuiya ya Kikristo Tanzania kupitia Mkutano Mkuu wa 29 uliofanyika Julai 2017, pamoja na mambo mengine ulipitisha Mkakati wa miaka mitano wa CCT kujitegemea kiuchumi.  Mojawapo ya mapendekezo ya kimkakati ni kuandaa na kufanya uchangiaji wa njia ya Harambee.  Kwa msingi huo, Mkutano wa Halmashauru Kuu ya 52 iliyokutana tarehe 12-13/7/2018 Dodoma ilipitisha andiko kuhusu Harambee ya Kitaifaambayo ilifanyika Julai 2019. 

Zoezi la Kuchangia juu ya Kitega uchumi hiki bado linaendelea, Hivyo wewe kama mdau/Rafiki unaombwa kutoa mchango wa kuchangia kiasi chochote ulichonacho.

Unaweza kuchangia kupitia  njia zifuatazo

 

Bank:

Jina la Akaunti: CCT Jengo

Namba za Akaunti CRDB Account No. 0150281796400

Asanteni sana na Mungu awabariki .

Mchg. Can. Moses Matonya

KATIBU MKUU