Kikundi cha Amani kilianza mwaka 2010 kikiwa na wanachama 30 hadi sasa kina wanachama hai 25
Anasimulia mwenyekiti wa kikundi hicho Marry Chacha oringa, Tulianza kuweka na kukopa, tulikuwa na masha duni, tulipopata elimu ya vikoba, tulianza kuweka na kukopa kidogo dogo kupitia biashara zetu ndogondogo.
Kuanzia mwaka 2022 tulianza kuona mabadliko baada ya kuanzisha mradi wa viti 200 vya kukodisha, na baadae tukaanzisha mradi wa mizinga ambapo hadi sasa tuna mizinga kumi na mizinga sita sasa ina nyuki (Agost 2025).
Pia tuna mradi wa ujenzi wa nyumba ya ofisi, Kwa sasa bado tunatumia majengo ya shule ya msingi kwa ajii ya vikao vyetu (chumba cha darasa). Hivyo tunajenga ofisi yenye eneo la kufanyia vikao na kutunzia kumbukumbu zetu.
Tumeanzisha mradi wa mashine ya kukoboa na kusaga ambao tunaendelea na mchakato wa kuisimaka.
Tuna mradi wa kutunza mazingira ambapo tumepanda miti 2,000 katika chanzo chetu cha maji (maarufu kama Rambo) ambapo tunafugia samaki.
Tulianzisha mradi wa samaki ambao sasa umeweza kutupanua, tunavuna tunapata hela na kupitia huu mradi ndipo tumepata hela ya kujengea ofisi yetu.
Tumeboresha utunzaji wa mzingira ya mradi wetu wa samaki kwa kutenga eneo la kunyweshea mifugo, na bwawa letu linabaki kuwa salama. Tumetengeneza eneo la kunyweshea mifugo kama ng’ombe, na sasa wameshazoea eneo hilo na hawaharibu bwawa letu. Tumewatengenezea watu hususani akina mama bomba la kuchota maji ambayo yanapatikana masaa yote, lengo wasiingie katika bwawa letu la samaki. Tungeacha watu na mifungo watumie bwawa tusingefanikiwa, bwawa lingeharibiwa na tusingepata samaki, amesimulia mwenyekti huyo.
Tumetengeneza ajira kwa mtu ambaye anatusaidia kuvua samaki ambapo kila akivuna tunamilipa.
Kwa mwaka tunavuna mara tatu, kuna mda tunapata vizuri mfano mwezi wa sita hadi mwezi wa nane tunaweza kupata hata milioni saba . wakati wa mvua kama mwezi wa nne tunapata hela ndogo kama milioni moja, amesema.
MSAADA WA MADAWATI 13 SHULENI
Kupitia mradi huu wa samaki tumeweza kutoa msaada wa viti 13vyenye thamani ya Tsh 940,000 kwa shule ya msingi Kisangula. Mwenyekiti wa kikundi anasema, Uongozi wa shule ya Kisangula tumesaidiana hususani katika elimu tunayoitoa ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji kwa watoto wa kike. Hivyo tumeona turudishe fadhira, tumeondoa dhana ya mtoto wa kike asiyekeketwa haolewi, sasa tumewasomesha watoto na wameolewa. Hivyo tumeon ni vyema tulete zawadi ya viti kwa watoto, kwa kuwa wameanza kufuata nyayo za wakubwa wao. Na sasa tunategemea matokeo mazuri zaidi kwa watoto hawa. Hii ni shukrani tu ambayo tumeamua kutoa, amesema mwenyekiti wa kikundi.
Kupitia ofisi ya maendeleo ya jamii, bwana Bahati Manoti ni afisa maendeleo Simanjiro ambaye amepongeza kazi zinazotekelezwa na CCT kwani CCT imekuwa chachu ya maendeleo katika Wilaya ya Serengeti. Hivyo tuendelee kuimarisha uhusiano wetu katika kuihudumia jamii.
Samweli maiko mwanafunzi wa shule ya msingi kisangula, darasa la nne ni mwanaklabu ya CCT katika shule hii, ameshukuru sana yeye kama kiongozi wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani ukeketaji. Amesem hii ni kwa sababu mmetutia moyo kwa kuwa tulikuwa tunakaa kwa kubanana hivyo wengine kutoona umuhimu wa kuja shuleni. Baada ya msaada huu tutasoma kwa uhuru, thatutabanana tena, Tutaongeza juhudi katika masomo na tutafanya vizuri.
Sophia mchomvu ni mratibu CCT katika Wilaya ya Serengeti
Ameeleza umuhimu wa vikundi ikiwa ni kuinua kipato na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia. Madawati haya ni chachu kwa mtoto wa kike aweza kusoma nakuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Amesema kikundi cha amani ni moja ya vikundi 50 vinavyofanya vizuri ndani ya wilaya ya Serengeti na leo wamegawa madawati 13 wakishirikiana na CCT.
Ni furaha yangu kwa kuwa tukio la leo limesababishwa kuanzishwa kwa kikundi kipya ambacho kimetokana na wenza wa wanakikundi ambao wameshiriki tukio hili, amesema. Baada ya kuona mafanikio makubwa ndani ya kikunsincha amani, wameamua kuanzisha kikundi chao, wamefanya uamuzi huo kupingana na fikra hasi zilizoko kwenye jamii.
Nawashukuru CCT na idara ya maendeleo kwa namna mnavyotupa ushirikiano katika shughuli zetu za vikundi hapa Serengeti.
MMOJA WA WANAKIKUNDI KIPYA ANASIMULIA
Naitwa Amos Lachau ni mwenza wa mwanakikundi cha Amani hapa Kisangura baada ya kuona mambo mazuri ndani ya kikundi, nimeamua kuungana na wenzangu ndani ya tukio la leo kuanzisha kikundi chetu. Nimeona namna ambavyo wanasaidia katika upande wa elimu, kusaidiazana wenyewe kwa wenyewe. Kwa hali hiyo tumeshawishika kuunda kikundi kama hiki ili tuendelee tuweze kupanuka kimawazo na kiuchumi katika familia zetu.
Anasema hii ni njia mojawapo ya kusaidizana, nashukuru CCTkuanzisha vikundi hivi vya pamoja, natarajia kuona mpango endelevu katika kikundi chetu. Kama tumeweza kupata samaki wakubwa katika kikundi hiki, samaki ambao tulikuwa tunawapata kutoka Mwanza, basi kuna umuhimu wa kujiunga na kikundi.
Esther Muhagachi
Ni mratibu wa CCT idara ya wanawake, amefurahishwa na kazi mbalimbali zinazofanywa na kikundi, akiwapongeza wanakikundi kwa kazi kubwa wnayofanya.
Amesema CCT inafanya kazi ya kutoa elimu kwa kuwawezesha watu kutambua fulsa zilizoko katika maeneo yao na kuzichangamkia. Tumeungana na kikundi hiki kutoa zawadi ya madawati ikiwa ni jitihada ya kuwaunga mkono. Nitoe wito kwa wanavikoba wengine kuiga kile ambacho kimefanywa na kikundi hiki cha kutoa zawadi ya madawati shuleni, pamoja na kupanda miti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.
Serikali iimarishe ulinzi wa eneo la ufugaji wa samamii kuzuia wezi ambao wanaiba samaki wakati wa usiku. Atakayekamatwa akiiba atozwe faini na iingizwe kwenye mfuko wa kikundi. Nimefurahi kuona kikundi kipya kinazaliwa leo katika tukio hili, huu umekuwa wito wetu katika kuhamasisha wananchi kuunda vikundi hususani wanapojionea mafanikio mazuri kupitia vikundi vingine.
Scroll to Top