KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI JUU YA USAWA KWA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI

Kongamano la Viongozi wa dini mbalimbali linalowahusisha TEC,CCT &BAKWATA juu ya usawakatika huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma za Bima ya afya, ulipaji kodi, elimu, uchumi n.k

Baadhi ya wajumbe wakiongoza mjadala wa nini kifanyike kuhakikisha watu wote wanapata huduma kwa usawa, hususani kulinganisha huduma za kijamii kwa walioko vijijini na mjini

Kongamano hili limehudhuliwa na wawakilishi wa makatibu wakuu wa TEC,CCT &BAKWATA

  1. Dr. Camillius D.N Kassala TEC
  2.  Bi. Clotilda Ndezi CCT
  3. Shk Mohamed Khamis Said BAKWATA

Baadhi ya washiriki waliochangia mbinu au njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa usawa hasa maeneo ya mjini na vijijini.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais –TAMISEMI imeboresha mfumo wa utoaji huduma ya Bima ya Afya CHF ambapo imekuwa ICHF kwa sasa na ipo ngazi ya Mkoa na sio ngazi ya Wilaya kama ilivyokuwa awali.Hayo yameelezwa na Mratibu wa ugawaji huduma za afya Dr. Boniphace Richard wakati akiwasilisha maada kwenye kongamano hilo.

Wadau wameshauri swala la usawa lianzie katika ofisi za viongozi wenyewe , uaminifu katika kazi na kuzingatia heshima ya uumbaji wa binadamu, kuondoa matabaka, kuwajibika kwenye majukumu na elimu ya kutosha kupitia nyumba za ibada.

Uwiano wa bajeti ya serikali kwa wizara ya

Bw. Daniel Mugizi Mkuu wa kitengo cha Utawala na Fedha kutoka taasisi ya SIKIKA 

Amefafanua vizuri uwiano wa bajeti ya serikali kwa wizara ya Afya na mgawanyo wa bajeti hiyo kwa vitengo mbalimbali ndani ya wizara hiyo.

Wadau wamehoji juu ya mgawanyo wa bajeti ndani ya wizara kama unazingatia  usawa ikiwemo upatikanaji wa vifaa tiba, madaktari na Vituo vya afya kwa maeneo yote ya mjini na vijijini. Nje ya bajeti ya wizara serikali pia kuendesha huduma za Afya hutegemea msaada kutoka kwa wafadhili ambapo wengi wao hutoa fedha moja kwa moja kwa mashirika yanayotoa huduma ndani ya nchi.

Wizara ya Afya pia hutegemea fedha toka sekita/wizara zingine kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma zake.

Madini ni vyanzo vikubwa vya mapato ndani ya nchi yetu, Je tumeweka akiba juu ya mapato yanayopatikana kutokana na madini haya? Je Tanzania haina makampuni yanayoweza kusimamia uchimbaji wa madini hayo? Ni baadhi ya maswali ambayo wajumbe walihoji juu ya utetezi wa kizazi kijacho ili pawepo na akiba kama ilivyofanyik kwa mataifa yaliyoendelea.

Leave a Reply