MKUTANO WA VIONGOZI WAKUU WA DINI KUHUSU UKIMWI NA UNYANYAPAA.


Mkutano wa viongozi wa dini kuhusu UKIMWI na unyanyapaa umefanyika Tar 19-20 February 2020 katika ukumbi wa Mount Meru Hotel Jijini Arusha

Kwa nini unyanyapaa:

unyanyapaa ni hali ya kutengwa au kubaguliwa kwa sababu ya hali fulani au ugonjwa mbaya  uliompata mtu.

Hali ya unyanyapaa husababishwa na hofu ya jamii kuhusu matokeo ya hali hiyo kwa wengine na hasa kwa kukosa taarifa sahihi kuhusu tatitzo husika na athari yake kwa wengine.

Jinsi ya kukabiliana na unyanyapaa:

1.         Kuwa na program maalum ya kutoa elimu sahihi kwa jamii kupitia forum mbalimbali zinazogusa jamii kama vile mikutano ya dini, kupitia taasisi za elimu, vyombo vya habari, vilabu vya michezo vikindi vya sanaa, mikutano ya vijiji nk

2.         Elimu iambatane na kuhimiza / kutia moyo watu watambue hali zao za kiafya kwa njia ya kupima.

kupima afya sio utamaduni wetu, hivyo kunahitajika nguvu kubwa katika kuwashawishi watu wetu wawe tayari kupima.

3.         Kuwapo pia program madhubuti ya namna ya kukabiliana na matokeo ya watu kutambua hali zao, yaani matokeo ya kisaikolojia, kijamii, kiuchumi pamoja na tiba kwa wale wanaopata matokea chanya. ushauri nasaha katika ngazi zote za kutolea tiba, matibabu, lishe nk ni vipengele mhimu sana katika kukabili vita hivi.

4.         Kutoa elimu sahihi kuhusu kuzuia maambukizi mapya. Kubadili tabia ni wito mkuu zaidi kuliko mbinu zinginezo.

5.         Napendekeza pia kwamba vyombo hivi vya kupamabana na Unyanyapaa na ugonjwa wa ukimwi kwa ujumla, viende kukutana na makundi haya matano ya kidini moja moja kabla ya kuunda chombo cha pamoja.

Askofu Malekana

Leave a Reply