OMBI LA KUSHIRIKI HARAMBEE

Jumuiya ya Kikristo Tanzania kupitia Mkutano Mkuu wa 29 uliofanyika Julai 2017, pamoja na mambo mengine ulipitisha Mkakati wa miaka mitano wa CCT kujitegemea kiuchumi.  Mojawapo ya mapendekezo ya kimkakati ni kuandaa na kufanya uchangiaji wa njia ya Harambee.  Kwa msingi huo, Mkutano wa Halmashauru Kuu ya 52 iliyokutana tarehe 12-13/7/2018 Dodoma ilipitisha andiko kuhusu Harambee ya Kitaifa inayopangwa kufanyika Julai 2019.  Mgeni Rasmi wa Harambee hiyo alipendekezwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli;  ambaye alipewa mwaliko na amekubali kuwa         Mgeni  Rasmi atakayeshiriki kufunga Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 53 mwaka 2019 na Kisha Harambee ya Kitaifa ambapo yeye binafsi pia atachangia.

Hivyo wewe kama mdau/Rafiki unaombwa kushiriki harambee hiyo kwa kuchangia kiasi chochote ulichonacho.

Unaweza kuchangia kupitia  njia zifuatazo

 TIGO PESA

Namba:    0717656916

Jina:    CHRISTIAN COUNCIL OF TANZANIA

Bank:

Jina la Akaunti: CCT Jengo

Namba za Akaunti CRDB Account No. 0150281796400

Asanteni sana na Mungu awabariki .

Mchg. Can. Moses Matonya

KATIBU MKUU

Leave a Reply