Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili-Kijiji cha Kiziwa kata ya Kiroka Mkoani Morogoro.

Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zinaendelea katika mikoa yote, ambapo leo CCT kwa kushirikiana na shirika la TCRS wametoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kijiji cha Kiziwa kata ya Kiroka Mkoani Morogoro.


Eneo hili linakabiliwa na vitendo vya ubakaji hasa kwa watoto wadogo wengi wao wakiwa wanafunzi.
Washiriki wameweza kueleza vitendo vya ukatili vinavyotesa jamii yao.

Mzee Mchalichaly Msemaji wa TUPO Kiziwa Group amesema vyombo vya sheria vumekuwa vikipata changamoto ya kutoa maamuzi kwani pande zote mbilli (mshitaki na mshitakiwa) kukaa pamoja na kulipana pesa bila kushirikisha vyombo vya sheria, hii imefanya vitendo vya ubakaji viwe vingi katika maeneo haya.

Mratibu wa Kitendo cha wanawake CCT, Bi Esther Muhagachi kwa kushirikiana na Mratibu wa Kutoa elimu kwenye jamii toka TCRS Bw. Gasper J Werema wameelimisha jamii hiyo namna ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo wamesisitiza kila mmoja kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili.
 Pia wamesisitiza jamii kushirikisha vyombo vya sheria pale mtu anapofanyiwa vitendo hivyo.

Ugawaji wa vipeperushi toka CCT vya kupinga vitendo vta ukatili wa kijinsia ulifanyika ili wananchi waendelee kujifunza na kuelemishana wenyewe kwa wenyewe.


M/Kiti wa kijiji hicho Bwana Jasters Saimon ameshukuru sana CCT na TCRS  kwa kutoa elimu na kuomba kuendelea kuleta mafunzo haya ili wananchi waendelee kupata uelewa  wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kushirikisha vyombo vya sheria.

Leave a Reply