UWAKALA WA BIMA

HABARI NJEMA

Jumuiya ya Kikristo Tanzania katika muendelezo wa mpango wake wa kujitegemea kiuchumi, imeanzisha Mradi wa Uwakala wa Bima kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa jina la CCT INSURANCE AGENCY, ulioanza  Desemba 2018.

Mradi huu unaendeshwa kutoka Makao Makuu CCT Dodoma na katika ofisi  zinazofunguliwa  nchini kote chini ya Uongozi wa CCT Mikoa. Hivyo ukiwa kama mdau muhimu kwetu unakaribishwa sana kupata huduma zote za Bima, kwa haraka, ubora na uhakika.

HUDUMA ZETU

Zifuatazo ni Bima zinazotolewa nasi:-

 • Bima ya magari na vyombo vya moto

Aina za Bima ya magari:-

 1. Bima Ndogo (Third Party Only) “ambayo ni ya lazima kwa kila chombo Kisheria”
 2. Bima Kubwa (Comprehensive/ Owner Cover)
 3. Bima ya Kati (Third Party Fire and Theft)
 4. COMESA Yellow Card
 5. Bima ya nyumba ya makazi dhidi ya ;
 6. Moto, radi, mlipuko, moto chini ya ardhi.
 7. Tetemeko la ardhi, kimbunga, mafuriko.
 8. Kuangukiwa na mti au matawi yake.
 9. Wizi au jaribio la wizi
 10. Kinga ya majanga ya Biashara
 11. Bima ya moto na majanga kama milipuko,wizi, vyombo vya angani n.k
 12. Kinga ya Biashara (kulinda faida ambayo ungeendelea kuipata kama janga lisingetokea).
 13. Bima ya fedha (Money insurance).
 14. Bima ya maisha (Life insurance).
 15. Bima ya Mitambo maalumu (Engineering), mfano kompyuta n.k.
 16. Mizigo isafirishwayo.

MAHALI TULIPO

Makao yetu makuu ni Jijini Dodoma, Barabara ya Hospitali, Ghorofa ya kwanza Jengo la CCT Church House, karibu na Mackay House / Mkapa House.

MAWASILIANO

Kupata huduma/ maulizo

Tupigie simu kwa simu nambari +255 767 103767,  +255 684 230250, +255 756 163140.

Application Form

Leave a Reply