UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

MABADILIKO YANAANZA NA MIMI

Kuanzia tarehe 25 Novemba, siku ya kwanza ya kampeni ya Kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto ambapo uzinduzi wake umefanyika katika ukumbu wa Julius Nyerere International Convention Centre Dar es Salaam.

Kampeni ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni wakati wa kutafakari juu ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

Huu ni wakati wa kutafakari, kupaza sauti na kuelimisha jamii kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia, madhara yake, na hatua za kuchukua kukabili vitendo hivyo.

Kongamano hili limezinduliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson na kuhudhuliwa na wadau wengi akiwemo Balozi wa Denmack Bi. Mette Norgaard Spandet na Mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa Bw. Zlatan Milisic na Katibu mkuu wizara ya Afya,Maendeleo,Jinsia Wazee na Watoto Dr. John Jingu. Katika uzinduzi huu baadhi ya viongozi wa CCT walipata nafasi ya kushiriki na kupata nafasi ya utambulisho, viongozi wa Dini ni chachu ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwani wana ushawishi mkubwa katika nyumba zao za ibada.

Mgeni rasmi aliweza kuzindua programu (App) iitwayo GBV Taarifa ambayo itatumika kutolea taarifa za vitendo vya ukatili. Ampapo mhanga ataweza kutoa taarifa zake na eneo alipo hivyo kumrahisishia yeye kupata msaa wa haraka.

CCT kupitia Kurugenzi ya Programu za Maendeleo na Utetezi walifanikiwa kutoa huduma ya  madhara ya ukatili na kijinsia na namna ya kukemea vitendo vya ukatili.Picha ni mkurugenzi wa kurugenzi hiyo akitoa elimu kwaliotembelea banda

Katika uzinduzi huu Mkurugenzi wa WILDAF Tanzania Bi Anna Meela Kulaya alifanikiwa kutembelea banda la CCT na kujionea shughuli mbalimbali za utetezi zinazofanywa na CCT

Sehemu zingine ambazo huduma ya kupinga vitendo vya ukatili hufanyika ni

 Women in Law and Development in Africa (WiLDAF) ambapo unaweza kupiga namba bila malipo  0800780070, Legal and Human Right Centre (LHRC) 0800750035, Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA)  0700751010, Legal Aid Centre (WLAC) 0800780100, Tanzania Youth Alliance (TAYOA) operates the National Health (Afya) AIDS Helpline.

UKIFANYIWA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA CHUKUA HATUA ZIFUATAZO:

Ripoti tukio la ukatili katika madawati ya polisi ya kijinsia (Police Gender Desks) yanayopatikana kwenye vituo vya polisi, Ofisi za ustawi wa jamii, Vituo vya msaada wa kisheria.

Kabla ya kuahirisha Uzinduzi huu CCT waliweza kupata picha ya pamoja na mgeni rasmi , Mabalozi na wadau wengine.

Baada ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia  CCT walifanikiwa kutembelea shule ya Mtoni Maalum Iliyopo Dar es Salaam  na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo sukari,sabuni,dawa za meno na miswaki, unga wa ugali,mafuta ya kupikia na vifaa maalum kwa watoto wa kike

Leave a Reply