WARSHA YA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WALIOGOOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI MKUU – 2020 KATIKA MKOA WA SONGWE

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (C.C.T) kupitia Mradi wa Mwanamke Jasiri kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) iliandaa Warsha ya Wanawake kutoka katika vikundi vya Wanawake Wajasiriamali kutoka katika Halmashauri za Wilaya Mbozi, Ileje, Momba pamoja Halmashauri ya Mji wa Tunduma waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Mkoani Songwe. Warsha ilifanyika katika ukumbi wa Kal (Kal Hall) uliopo Vwawa Wilayani Mbozi.

MALENGO YA WARSHA

Malengo ya Warsha yalikuwa yafuatayo:-

  • Kuwaelimisha juu ya Sheria na Utaratibu wa kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi na changamoto za wanawake kushiriki katika Uchaguzi.
  • Kuwaelimisha Wanawake katika vikundi vya ujasiriamali juu ya kukabiliana na changamoto za kibiashara.

 Mafunzo haya yalifunguliwa na Afisa Biashara kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe akiwa ameambatana na Afisa Maendeleo ya Jamii. Pia ilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Programu ya Maendeleo na Utetezi Bi. Clotilda T. Ndezi, Mratibu wa Programu ya Mwanamke Jasiri Bi. Christina V. Motto, Afisa Tathmini na Mipango na Ufuatiliaji Bw. Ndekirwa G. Urio pamoja na Afisa Uwezeshaji Uchumi Bw. Azgard S. Chamlungwana.  

Watoa mada  katika mafunzo haya ni watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Songwe ambao ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Mussa Mwanja na Afisa Biashara Bw. Lazaro J. Melchizedek

Mratibu wa Programu akiwaelekeza Washiriki kuhusu tahadhari muhimu za kukabiliana na virusi vya corona.
Mkurugenzi wa Program ya Maendeleo na Utetezi akielezea kuhusiana na Jumuiya ya Kikristo Tanzania na Mradi wa Mwanamke Jasiri wakati wa Warsha.
Afisa Biashara akitoa mafunzo kwa washiriki.
Afisa Maendeleo akitoa elimu kwa Washiriki katika Warsha.

Washiriki wa Warsha wakiwa katika picha ya pamoja na Wawezeshaji pamoja Watenda kazi wa C.C.T

Leave a Reply