Warsha ya kuwajengea uwezo wanawake waliothubutu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Mkoa wa Dodoma.

Warsha ya kuwajengea uwezo wanawake waliothubutu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Mkoa wa Dodoma.

Lengo kuu ni kuwaelimisha juu ya sheria na Utaratibu wa kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi na changamoto za wanawake kushiriki katika chaguzi. Pia Kuelimishwa juu ya kukabiliana na changamoto za kibiashara kwa vikundi vya wanawake.

 Mafunzo haya yamezinduliwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  Mchungaji Canon Moses Matonya na  kuhudhuliwa na  viongozi mbalimbali toka CCT akiwemo Afisa Utawala na Rasilimali watu Bw. Godlisten Moshi na Mkurugenzi wa Programu za Maendeleo na Utetezi Bi Clotilda Ndezi. Watoa mada  katika mafunzo haya ni watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma ambao ni Mratibu wa Uchaguzi Bw.Nathalis L Linuma, Afisa Maendeleo Bi Honoratha M Ruegas na Afisa Biashara Bi Prisca M Dugilo.

Warsha hii imewezeshwa na CCT kupitia mradi wa Mwanamke Jasiri (Strong Woman Program) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD)

Katibu Mkuu CCT akitoa neno wakati wa Ufunguzi
Mkurugenzi wa programu za maendeleo na utetezi CCT akiwasilisha maada kwenye warsha
Afisa biashara akielimisha washiriki

Afisa Uchaguzi akiwasilisha maada kwa washiriki´╗┐
Afisa Utawala na Rasilimali watu akichangia jambo kwenye mkutano
Picha ya pamoja baada ya warsha

Leave a Reply