Rt. Rev. Dr. Fredrick
Shoo Chair Person
Rev.Can.Dr. Moses Matonya
General Secreatry
First slide Nyumba zinapangishwa-Dodoma CCT Insurance AgencyCCT INSURANCE AGENCY

TUNATOA BIMA ZA: Magari na vyombo vya moto, Nyumba ya makazi, Majanga ya Biashara, Moto, , Fedha, Maisha, Mitambo maalumu. Mizigo isafirishwayo

Tupigie kupitia 0693490180

Kama ungependa kuhudumiwa na sisi tunaomba ujaze taarifa zako hapa

Karibu Tukuhudumie »


Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Nelson Kisare ametoa elimu kwa watumishi wa CCT namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya CORONA. Kama Kanisa ametoa mwongozo wa kufuata ambao unapatikana 2 Nyakati 7:14 Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Askofu amewasihi watumishi kufuata taratibu zinazotolewa na wataalamu wa Afya namna ya kukabili virus hivyo. Elimu hiyo imetolewa leo Tar 27 Agosti 2021 wakati akiongoza ibada fupi ya asubuhi katika ofisi za CCT Makao Makuu Dodoma.

Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ulipofanyika tarehe 8-9/7/2021 katika kituo cha Mafunzo ya Wanawake CCT Morogoro pamoja na mambo mengine ulifanyika uchaguzi wa Viongozi wake watakao ongoza kwa kipindi cha miaka 4 ijayo. Waliochaguliwa ni hawa wafuatao;- Baba Askofu Dkt, Fredrick Shoo - Mwenyekiti( wa pili kutoka kilia); Baba Askofu Dkt. Stanly Hotay - Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti ( wa tatu kutoka kulia); Baba Askofu Dkt. Alinikisa Cheyo- Makamu wa Pili wa Mwenyekiti ( wa kwanza kutoka Kushoto) na Baba Mchg, Canon Dkt. Moses Matonya - Katibu Mkuu ( wa kwanza kulia). Picha mbalimbali baada ya tukio la kuwapata viongozi wapya zimeambatanishwa