More details

Kikao cha Viongozi wa Vijana kutoka katika makanisa wanachama CCT Jiji la Dodoma

Kikao cha Viongozi wa Vijana kutoka katika makanisa wanachama CCT Jiji la Dodoma wamekutana leo tar 27/8/2022 katika Kanisa Kuu la Anglikana. Moja ya Mpango wa kuwakutanisha vijana hawa ni kuongeza ushirikiano na mshikamano , kutengeneza fulsa kupitia makongamano na semina za ujasiliamali. Kikao hiki ni mkakati wa kuunganisha vijana toka makanisa wanachama CCT, Kila mmoja asiachwe nyuma. Kila Mkoa utawekewa utaratibu wa kuwa na uongozi wa Vijana, pia kila wilaya. Hii yote ni kuimarisha umoja miongoni mwa vijana wa makanisa wanachama. Katika kikao hiki viongozi wa vijana kwa mkoa wa Dodoma wameweza kuchaguliwa kama ifuatavyo Mwenyekiti Issack Yohana kutoka Kanisa Kuu la Angalikana , Makamu mwenyekiti Pendo Malonja kutoka kanisa la AICT ipagala, Katibu Simoni Mbwaga kutoka kanisa la Moravian Iringa road, Katibu Msaidizi Glory Phocus kutoka Kanisa la Mennonite Iringa road, Mhazini Bosco Luitiko kutoka kanisa la Moravian Iringa Road. Kikao kimeongozwa na CCT kupitia Idara ya Umisheni na Uinjilisti chini ya Mchg. David Kalinga