More details

Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCT USCF TAIFA 2022

Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCT USCF TAIFA kilifanyika 12 Nov 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtumba Jijini Dodoma Kupitia kikao hiki imekuwa ni nafasi ya kujua maendeleo ya kila tawi la USCF katika Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Pia imekuwa sehemu ya kuweka mikakati ya kuimarisha chombo hiki. Kikao hiki kimehudhuriwa na viongozi wa CCT akiwemo Mkurugenzi wa Utume na Uinjilisti Mchg David Kalinga, Wachungaji wa Chaplaincy, Viongozi wa USCF Taifa, Mikoa, Wilaya na Matawi mbalimbali.