KUHUSU SISI

Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo inajulikana kwa kifupi kama CCT (Christian Council of Tanzania), ni Taasisi mwavuli inayowakilisha Umoja wa Madhehebu ya Kikristo ya Kiprotes- tanti Tanzania. Kwa sasa CCT inaundwa na Makanisa mbalimbali Wanachama na Vyama vya Kikristo au vyenye mwelekeo wa kikanisa kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Soma Zaidi

Taasisi hii ilianzishwa rasmi tarehe 23 Januari, 1934 kutokana na maono ya Wamisionari kutoka Kanisa Anglikana, Kanisa la Moravian na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri. Wamisionari hawa walipata maono ya kujenga umoja kati ya makanisa wanachama ambao utajihusisha na masuala mbalimbali ya kiimani, kimaendeleo na kijamii.. Muungano huu ulijulikana kwa jina la Kiingereza, Tanganyika Missionary Council (TMC) ". Mnamo mwaka 1964 Mungu aliwapa maono watumishi wake Baba Askofu Stephano Reuben Moshi (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania), Baba Askofu Theofilo Kisanji (Kanisa la Moravian Tanzania) na Baba Askofu Mkuu John Sepeku (Kanisa Anglikana Tanzania) kubadilisha usajili wa TMC kuwa Christian Council of Tanzania (CCT), jina linalotumika hadi sasa. Idadi ya Makanisa yaliyopo chini ya CCT imekuwa ikiongezeka kutoka Makanisa matatu (3) ya mwanzo mwaka 1934 hadi kufikia makanisa ya Kiprotestanti kumi na mbili (12) yaliyopo mwaka 2024

MAKANISA WANACHAMA CCT

  • i. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
  • ii. Kanisa Anglikana Tanzania (KAT)
  • iii. Kanisa la Moravian Tanzania (MCT)
  • iv. Africa Inland Church Tanzania (AICT)
  • v. Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT)
  • vi. Jeshi la Wokovu (Salvation Army)
  • vii. Kanisa la Baptist Tanzania (BCT)
  • viii. Presbyterian Church of East Africa (PCEA)
  • ix. Kanisa la Mungu Tanzania
  • x. Kanisa la Biblia Tanzania
  • xi. Kanisa la Uinjilisti Tanzania
  • xii. Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi (KIUMA)

VYAMA VYA KITUME WANACHAMA CCT

  • i. Bible Society of Tanzania (BST)
  • ii. Tanganyika Christian Refugees Service (TCRS)
  • iii. Young Men’s Christian Association (YMCA)
  • iv. Young Women’s Christian Association (YWCA)
  • v. Africa Evangelistic Enterprise (AEE)
  • vi. Life Ministry Tanzania
  • vii. Emmanuel International
  • viii. Summer Institute of Linguistics (SIL)
  • ix. Compassion International Tanzania
  • x. Dodoma Christian Medical Centre (DCMC)
  • xi. Mission Aviations Fellowship (MAF)
  • xii. Scripture Union
  • xiii. Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC)
  • xiv Amazing Grace

WasilianaNasi

Jumuiya ya Kikristo Tanzania

Anwani

S.L.P 1454 Dodoma, PostCode 41103

Simu

+255262324445

Barua Pepe

info@cct.or.tz

Loading
Ujumbe wako umetumwa. Asante sana!