

Ask. Dkt.Stanley Hotay
Mwenyekiti

Mchg.Can.Dkt. Moses Matonya
Katibu Mkuu
Kuhusu CCT
Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo inajulikana kwa kifupi
kama CCT (Christian Council of Tanzania), ni Taasisi mwavuli inayowakilisha
Umoja wa Madhehebu ya Kikristo ya Kiprotes- tanti Tanzania. Kwa sasa CCT
inaundwa na Makanisa mbalimbali Wanachama na Vyama vya Kikristo au vyenye mwelekeo
wa kikanisa kutoka Tanzania Bara na Visiwani. Taasisi hii ilianzishwa rasmi
tarehe 23 Januari, 1934 kutokana na maono ya Wamisionari kutoka Kanisa
Anglikana, Kanisa la Moravian na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri. Wamisionari
hawa walipata maono ya kujenga umoja kati ya makanisa wanachama ambao utajihusisha na masuala mbalimbali ya kiimani,
kimaendeleo na kijamii. Muungano huu ulijulikana kwa jina la Kiingereza, Tanganyika Missionary Council
(TMC).
Mnamo mwaka 1964 Mungu aliwapa maono watumishi wake Baba Askofu
Stephano Reuben Moshi (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania), Baba
Askofu Theofilo Kisanji (Kanisa la Moravian Tanzania) na Baba Askofu Mkuu John
Sepeku (Kanisa Anglikana Tanzania) kubadilisha usajili wa TMC kuwa Christian
Council of Tanzania (CCT), jina linalotumika hadi sasa. Idadi ya Makanisa
yaliyopo chini ya CCT imekuwa ikiongezeka kutoka Makanisa matatu (3) ya mwanzo
mwaka 1934 hadi kufikia makanisa ya Kiprotestanti kumi na mbili (12) yaliyopo
mwaka 2024
Dira ya CCT
Dhamira ya CCT
Tunu za CCT
Kuwa chombo cha Ki-ekumene cha Kikristo chenye kuleta maendeleo kamilifu na endelevu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.
Kudumisha umoja katika mwili wa Kristo na kuunganisha nguvu katika kutatua changamoto na kutumia fursa zilizopo kuleta maendeleo kamilifu na endelevu kwenye jamii.
Uwakili, Upendo na Huruma,Uwazi na Uwajibikaji, Umoja, Uaminifu na Uadilifu,Kuaminika na Uaminifu, Ubora na Taaluma, Kujitolea.


Programu za Maendeleo na Utetezi
Wafanyakazi wa CCT walifanya kikao cha kimkakati na washirika wetu kutoka Bread for the World (BftW), Ujerumani.
Mkutano huo ulilenga kukagua maendeleo yaliyofikiwa katika Mradi wa Elimu ya Uraia na Mradi wa Utetezi wa Kanisa na Uwezeshaji Vijana. Majadiliano pia yalilenga katika kuimarisha ushirikiano wetu tunapojiandaa kwa awamu inayofuata ya mipango hii yenye matokeo.”

Management Team

Godlisten Moshi
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu
ahr@cct.or.tz

Clotilda Ndezi
Mkurugenzi wa Programu za Maendeleo na Utetezi
cndezi@cct.or.tz

Rev David Kalinga
Mkurugenz wa Umisheni jna Uinjilisti
dkalinga@cct.or.tz

Beatrice Dengenesa
Mkurugenzi wa Uwekezaji
bdengenesa@cct.or.tz

Emma Mashauri
Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Wanawake Morogoro (MWTC)
director@cct-mwtc.co.tz

Boazi Kitaja
Mkurugenzi – Wakala wa Makanisa (WAMA).
director@wama-cct.org

Urio Ndekirwa
Afisa Mipango, Ufuatiliaji na Mafunzo
pme@cct.or.tz

Etanga Kajanja
Mhasibu Mkuu
finance@cct.or.tz

Grace Mayengo
Mkaguzi wa Ndani
auditor@cct.or.tz
Wadau wetu
Wasiliana nasi
Simu
+255 26 232 4445
gs@cct.or.tz
Anwani
CCT Head Quarter is in Dodoma
Church House
Along Hospital Rd.
Between 8th and 9th Rd.
Postcode 41103
P.O Box 1454,
Dodoma – Tanzania
Makanisa Wanachama CCT
Vyama Vishiriki CCT
- Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
- Kanisa Anglikana Tanzania (KAT)
- Kanisa la Moravian Tanzania (MCT)
- Africa Inland Church of Tanzania (AICT)
- Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT)
- Jeshi la Wokovu (Salvation Army)
- Kanisa la Wabaptist Tanzania (BCT)
- Presbyterian Church of East Africa (PCEA)
- Kanisa la Mungu Tanzania
- Kanisa la Biblia Tanzania
- Kanisa la Uinjilisti Tanzania
- Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi (KIUMA)
- Bible Society of Tanzania (BST)
- Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS)
- Young Men’s Christian Association (YMCA)
- Young Women’s Christian Association (YWCA)
- Africa Evangelistic Enterprise (AEE)
- Life Ministry Tanzania
- Emmanuel International
- Summer Institute of Linguistics (SIL)
- Compassion International Tanzania
- Dodoma Christian Medical Centre Trust (DCMCT)
- Mission Aviations Fellowship (MAF)
- Scripture Union
- Soma Biblia
- Amazing Grace
- Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC)