Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo inajulikana kwa kifupi
kama CCT (Christian Council of Tanzania), ni Taasisi mwavuli inayowakilisha
Umoja wa Madhehebu ya Kikristo ya Kiprotes- tanti Tanzania. Kwa sasa CCT
inaundwa na Makanisa mbalimbali Wanachama na Vyama vya Kikristo au vyenye mwelekeo
wa kikanisa kutoka Tanzania Bara na Visiwani. Taasisi hii ilianzishwa rasmi
tarehe 23 Januari, 1934 kutokana na maono ya Wamisionari kutoka Kanisa
Anglikana, Kanisa la Moravian na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri. Wamisionari
hawa walipata maono ya kujenga umoja kati ya makanisa wanachama ambao utajihusisha na     masuala             mbalimbali      ya     kiimani,
kimaendeleo na kijamii. Muungano huu ulijulikana        kwa  jina  la      Kiingereza,                 Tanganyika Missionary Council
(TMC).

 

Mnamo mwaka 1964 Mungu aliwapa maono watumishi wake Baba  Askofu 
Stephano Reuben Moshi (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania), Baba
Askofu Theofilo Kisanji (Kanisa la Moravian Tanzania) na Baba Askofu Mkuu John
Sepeku (Kanisa Anglikana Tanzania) kubadilisha usajili wa TMC kuwa Christian
Council of Tanzania (CCT), jina linalotumika hadi sasa. Idadi ya Makanisa
yaliyopo chini ya CCT imekuwa ikiongezeka kutoka Makanisa matatu (3) ya mwanzo
mwaka 1934 hadi kufikia makanisa ya Kiprotestanti kumi na mbili (12) yaliyopo
mwaka 2025

Scroll to Top