Utume na Uinjilisti

Jumuiya ya Kikristo Tanzania, kwa kuzingatia utume wake, inafanya shughuli mbalimbali za Kiroho na Kimwili. CCT inatoa huduma za kiroho kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vikuu. Kwa shule za Msingi hutolewa Elimu ya Kikristo. Kwa upande wa Shule za Sekondari na Vyuo vya kati huduma za kiroho huratibiwa na chombo kinachoitwa Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) na katika ngazi ya Vyuo Vikuu huratibiwa na chombo kinachoitwa University Student Christian Fellowship (USCF).

CCT DAY

CCT Day kama ilivyokuwa ikifanyika kila mwaka, malengo yake makuu ni kudumisha umoja wa waumini wa makanisa wanachama; kuendelea kuitambulisha CCT na vyombo wake kwa Waumini wa Makanisa Wanachama; kuitegemeza CCT kwa sadaka maalumu inayotolewa ili kuendeleza shughuli za kitume na kijamii.

Kwa mwaka huu, CCT Day imeratibiwa kufanyika mwezi Mei. Kilele cha Maadhimisho hayo kitafanyika Tarehe 30 Mei 2021 katika mikoa yote nchi nzima. Maadhmimisho haya yatafanyika kwa shughuli mbalimbali zitakazoratibiwa kwenye ngazi ya Mikoa.

CCT inatoa wito kwa kila muumini kuchangia kwa kadiri ya Baraka za Mungu alizomjalia ili kufikia Malengo yake ya kujiimarisha kiuchumi kwa ajili ya kutekeleza shughuli zake za kitume na kijamii.  

Michango hii inaweza kutumwa ofisi za CCT Makao Makuu Dodoma kupitia benki ya CRDB akaunti namba: 01J1081943800 Jina CCT GS SPECIAL au kupitia ofisi za CCT katika Mikoa.

 “Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.” (Mithali 14:34) 

 

Scroll to Top