TUWAFIKIE WAHITAJI KWA UPENDO WA KRISTO

Watumishi kutoka CCT Makao Makuu Dodoma wametembelea wafungwa wa gereza Kuu la Isanga lililopo Mkoani Dodoma.

CCT

Katika Ziara hiyo wamefanikiwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo nguo, viatu, miswaki, sabuni, dawa ya meno, mafuta kujipaka na taulo za kike. Watumishi hao wamekuwa  na utaratibu wa kuwa na sadaka kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya huduma za kichungaji, kusaidia wahitaji kama yatima, wafungwa, wagonjwa na walemavu.

CCT

Mkurugenzi wa Utawala CCT Bw. Godlisten Moshi kwa niaba ya Katibu Mkuu Mchg. Can. Dkt Moses Matonya ametoa Neno la kuwatia moyo wafungwa kutoka kitabu cha Yeremia 29:11 " _Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani si ya mabaya, kuwapa tumaini siku zenu za mwisho"

CCT _

Naye Mkuu wa Gereza hilo Bw. Fumbuka  amepongeza sana Uongozi wa CCT kwa kuliona hilo na ameomba upendo huu uendeleee huku akisisitiza hata kwa mtu binafsi  kutembelea wafungwa hao.