More details

Mafunzo ya Utetezi na namna ya kuwasilisha taarifa zake

Cct yaungana na wadau wengine katika mafunzo ya utetezi na namna ya kuwasilisha taarifa zake yaliyofadhiliwa na NCA Mkoani Arusha Kuanzia Tar 8 -10 Juni 2022. Mafunzo hayo yamelenga mikakati mbalimbali za kuisaidia jamii juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, Ubaguzi, uvunjifu wa amani na mbinu za kuimarisha kilimo bora. CCT inatekeleza kazi za utetezi katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Mara ambapo imeweza kuokoa maisha ya watoto wanaotaka kukeketwa kwa ajili ya kuozeshwa mapema hivyo kukatisha ndoto zao. Kwa mwaka 2022 hadi sasa CCT imeweza kutoa elimu kwa watoto 2456 kupitia tamasha mbalimbali, clab mashuleni na sehemu za ibada, pia kupitia mijadala na wadau mbalimbali katika kutekeleza hayo.