Mission & Evangelism


Maadhimisho ya CCT DAY

Maadhimisho ya CCT DAY ambapo Kitaifa Ibada yamefanyika KKKT Usharika wa Moshi Mjini. Mwenyeji ni Mwenyekiti wa CCT Taifa Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo




Ibada ya uzinduzi wa Tawi la USCF Chuo cha Utumishi wa Umma Singida

Ibada ya uzinduzi wa Tawi la USCF Chuo cha Utumishi wa Umma Singida, ambapo tawi hili limezinduliwa na Mkurugenzi wa Umisheni na Uinjilisti CCT Mchg. David Kalinga. Ibada hiyo imeongozwa Mchg.James Jima Mhubiri wa neno akiwa katibu wa USCF Taifa Bw Aman Kwale ambapo ametukumbusha juu ya kukaa Kwa Bwana siku zote za maisha yetu Zab 27:1-4




CCT YASHIRIKI SIKU YA MAOMBI YA WANAWAKE DUNIANI

CCT imeungana na wanawake katika siku ya maombi duniani tarehe 4 Machi 2022 siku ya maombi ya Wanawake duniani yenye lengo la kuombea Amani na mambo mengine ambapo Ibada ilifanyika katika kanisa Kuu la KKKT Dodoma. Ibada iliambatana na maandamano.Maombi ya dunia kwa wanawake hufanyika kwa makanisa yote kwa lengo la kuwafanya walioshiriki kurudia Imani katika nafsi zao na pia wametumia siku hiyo kuiombea dunia




Uzinduzi wa maombi ya Kitaifa ( Tanzania National Prayer Breakfast)

Uzinduzi wa maombi ya Kitaifa ( Tanzania National Prayer Breakfast)ambayo yanafanyika hapa Dodoma Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center yamezinduliwa na na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako. Katika hotuba yake amepongeza waandaaji wa Kongamano hili kwamba linawajenga vijana kimaandili, kiimani na kuwafanya vijana kuwa wazalendo katika Taifa letu. Kabla ya kutangaza kufunguliwa Kwa Kongamano hilo Waziri alikariri maneno ya Mungu kama ifuatavyo: 1Yohana 2:14b Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. Mithali 20:29(a) "Fahari ya vijana ni nguvu zao....." Kongamano limeandaliwa na ushirikiano wa Viongozi wa Kikristo nchini kutoka TEC,CCT,CPCT na SDA kupitia Kingdom Leadership Network Tanzania.




Ibada ya uzinduzi wa Chaplaincy tawi la CCT-USCF katika chuo Kikuu Cha elimu ya Biashara (CBE) Campus ya Dodoma.

Ibada ya uzinduzi wa Chaplaincy tawi la CCT-USCF katika chuo Kikuu Cha elimu ya Biashara (CBE) Campus ya Dodoma. Mgeni rasmi katika ibada hii ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) Mchg Canon Dkt. Moses Matonya. Uzinduzi wa Chaplaincy umeambatana na kusimikwa Kwa mchungaji mlezi , Mchg Modest Pesha na Mwl. Mlezi Dorice Munuo




TUWAFIKIE WAHITAJI KWA UPENDO WA KRISTO

TUWAFIKIE WAHITAJI KWA UPENDO WA KRISTO Watumishi kutoka CCT Makao Makuu Dodoma wametembelea wafungwa wa gereza Kuu la Isanga lililopo Mkoani Dodoma. Katika Ziara hiyo wamefanikiwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo nguo, viatu, miswaki, sabuni, dawa ya meno, mafuta kujipaka na taulo za kike. Watumishi hao wamekuwa na utaratibu wa kuwa na sadaka kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya huduma za kichungaji, kusaidia wahitaji kama yatima, wafungwa, wagonjwa na walemavu. Mkurugenzi wa Utawala CCT Bw. Godlisten Moshi kwa niaba ya Katibu Mkuu Mchg. Can. Dkt Moses Matonya ametoa Neno la kuwatia moyo wafungwa kutoka kitabu cha Yeremia 29:11 " _Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani si ya mabaya, kuwapa tumaini siku zenu za mwisho" _ Naye Mkuu wa Gereza hilo Bw. Fumbuka amepongeza sana Uongozi wa CCT kwa kuliona hilo na ameomba upendo huu uendeleee huku akisisitiza hata kwa mtu binafsi kutembelea wafungwa hao.




Ibada maalumu ya Kongamano la Wachungaji wa Kanisa la Anglikana Tanzania.

Ibada maalumu ya Kongamano la Wachungaji wa Kanisa la Anglikana Tanzania. Moja ya kusudi la kongamano hilo ni maadhimisho ya miaka 50 ya Kanisa la Anglikana Tanzania na pia miaka 176 ya uinjilisti. Maadhimisho hayo yamefanyika leo Tarehe 26/9/2021 katika Chuo Kikuu cha St. Johns Tanzania-Dodoma.




Kikao cha Kupitia Mwongozo wa USCF katika vyuo vya elimu ya kati na vya elimu ya juu

Kikao cha Kupitia Mwongozo wa USCF katika vyuo vya elimu ya kati na vya elimu ya juu kimefanyika leo katika ofisi ya CCT Dodoma. Kikao hiki kimeongozwa na Mkurugenzi wa Umisheni na Uinjilisti Mchg. David Kalinga na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala CCT, Godlisten Moshi na Viongozi kamati kuu ya USCF na baadhi ya walezi na Wahadhiri wa vyuo vikuu. Neno la kuongoza kikao limetoka kitabu cha 1Kor. 14:40 Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu




Ibada ya kuweka wakfu kiwanja cha Chaplaincy ya CCT UDOM

Ibada ya kuweka wakfu kiwanja cha Chaplaincy ya CCT katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) imefanyika leo katika Mtaa wa Nghonghona UDOM ambapo ndipo Kanisa la Chuo Kikuu cha Dodoma litajengwa. Ibada hii imeongozwa na Mratibu wa Chaplaincies za CCT Mchg. David Kalinga mbaye ndie Mkurugenzi wa Utume na Uinjilisti CCT. Ibada hiyo imehudhuriwa na wanafunzi kutoka vitivo vyote katika chuo hicho ambao wako chini ya Makanisa wanchama CCT. Ujenzi wa chaple utaambatana na nyumba kwa ajili ya watumishi wa kuongoza Chaplaincy hiyo. Mwenyeji katika ibada hiyo alikuwa ni Mchg. Timothy Erasto Chimeledya ambaye ndie Chaplain wa UDOM




Mkutano Mkuu wa 31 wa CCT

Picha ya Pamoja kati ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan na Maaskofu wa CCT, Wakuu wa Makanisa wanachama CCT, Umoja wa wanawake CCT na Secretarieti ya CCT. Tukio hilo limefanyika baada ya hotuba ya Rais Katika Mkutano Mkuu wa 31 wa CCT




 


CHAPLAINCIES

UDSM

MIPANGO

SUA

MUCE

MZUMBE

UKWATA