CCT kupitia mradi wa Tuwajibike imetoa mafunzo ya MURU Kwa viongozi wa kamati ya uhamasishaji wa maendeleo na ufuatiliaji wa rasilimali za umma kwa Mikoa ambako mradi unatekelezwa.
MURU ni Mfumo wa Ufuatiliaji wa Rasilimali za Umma unaojulikana kwa lugha ya Kiingereza kama Public Expenditure Tracking Systems or Surveys (PETS) ambao ni dhana ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma inayokuza uwazi, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika kupanga, kutekeleza, kusimamia na kufuatilia rasilimali za umma.
Malengo ya mafunzo kwa viongozi wa kamati ni kupata elimu juu ya usimamizi wa rasmilimali za Umma, Kutambua nafasi zao katika maeneo wanayotoka ili tukawafundisha wananchi wengine.
Kama wanakamati wanapaswa kujua namna gani watashiriki na kuhamasisha wengine kwenye shughuli za maendeleo ambazo zinaanza na mikutano. Mafunzo haya yawawezeshe kusaidizana na viongozi wa maneo ili kuweza kusimamia na kuhakikisha miradi inatuletea maendeleo kwetu sisi na kwa vizazi vijavyo .
Leo tunaishi kwenye miundombinu iliyosimamiwa na waliopita, hivyo ni wajibu wetu kusimamia miundombinu iliyopo kwa ajili yetu na vizazi vijavyo. Hivyo washiriki wanapaswa kuwa macho, kuelewa ni mambo gani ya kusimamia na kuyafuatilia ili yaweze kuleta maendeleo.
Moja ya viongozi wa Serikali walioshiriki mafunzo haya Neema Ntibagwe, Afisa Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa NGOs Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma amesema CCT ni wadau ambao wamekuja kutuunga mkono kama seriakli katika maswala ya uwazi na uwajibikaji. Ninyi (Washiriki wa mafunzo) mnapaswa kuwa kiungo muhimu katika haya mafunzo kwa niamba ya vitongoji/vijiji mlivyotoka.
Mafunzo haya ni ya muhimu kwetu tuzingatie kitakachofundishwa, sisi ni mabalozi katika usimamizi wa raslimali, mhakikishe jamii ina uelewa mradihuu ili tuwe kitu kimoja katika kulinda rasilimali za umma, amesema. Ushirikiano ni muhimu katika utekelezaji, hivyo washiriki amewahimiza kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa kwa wadau hawa (CCT) kwa wakati.
Amewahimiza washiriki kutekeleza vizuri kinachofundishwa kwa ajili ya kufikia malengo ya mradi, akisema mradi ni wetu tuhakikishe malengo yanafikiwa.
Mikoa ambako mafunzo yanatekelezwa ni Tabora, Shinyanga, Kigoma na Pwani
Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Norway (Norwegian Church Aid (NCA))





