Kuelekea maadhimishi ya Kilele cha siku ya CCT (CCT DAY) Tar 26,Mei 2024 ambapo kitaifa yataadhimishwa Mkoani Mtwara Kanisa kuu la KKKT, CCT kupitia idara ya afya wamegawa taulo kwa watoto wa kike katika shule ya sekondari RahaLeo iliyoko Mtwara Mjini.
Taulo zenye gharama ya milioni nane zimegawiwa kwa wanafunzi wa kike 300. Katika zoezi hilo, Baba Askofu Dkt. James Almasi(Mwenyekiti wa CCT Lindi/Mtwara) amewasihi wazazi hasa wanaume/akina Baba kuona umuhimu mkubwa wa kuhakikisha watoto wa kike wanapata huduma bora ya hedhi salama.
Siku ya hedhi huadhimishwa tarehe 28 Mei kila mwaka.


