More details

Development Programs & Advocacy

CCT imetoa mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wajane Wilayani Mpwapwa. Mafunzo hayo yamezinduliwa na Mchg. Amos Zakayo toka Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa Idara ya maendeleo. Katika hotuba yake amewatia moyo wajane akiwasihi kujiona wa thaman kwa sababu Mungu akaaye mahali pake patakatifu, ni Baba wa yatima na mlinzi wa wajane. Baadhi ya vitu ambavyo vimeonekana kusababisha ongezeko la ukatiliwa kijinsia kwa wajane ni pamoja na uelewa mdogo (elimu ndogo) na umaskini. Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika katika ukumbi wa Kanisa la Anglikana Tanzania ambapo wajane wamehimizwa kuwa na ushirikiano miongoni mwao hasa wanapoona mwenzao yuko katika hali ya kunyanyaswa. Pia wamesisitizwa kuwatumia wasaidizi wa kisheria wa CCT ambao wanapatikana Wilayani hapo pindi wanapokumbwa na changamoto inayohitaji ushauri/msaada wa kisheria. Mafunzo yameendeshwa na CCT kupitia idara ya wanawake na watoto yakiongozwa na Mkurugenzi wa Programu za Maendeleo na Utetezi , Bi Clotilda Ndezi.