More details

Warsha ya kutathmini kazi za mwaka huu 2022 na kuandaa mpango kazi wa mwaka 2023

CCT kupitia idara ya Mipango, Tathmini na Ufuatiliaji imeratibu warsha ya kutathmini kazi za mwaka huu 2022 na kuandaa mpango kazi wa mwaka 2023. Kikao kazi hicho kilihusisha watumishi wote wa CCT makao makuu na vitengo vyake vya Wakala wa Makanisa WAMA na Kituo cha mikutano cha wanawake Morogoro(MWTC). Wakati wa ufunguzi Katibu mkuu wa CCT Mchg Canon Dkt. Moses Matonya alisisitiza umuhimu wa kushirikiana katika utekelezaji kwa kuwa kila mtu ni kiungo muhimu sana katika kuujenga mwili wa Kristo kupitia CCT. Aitha alisisitiza kuwa, Hatuwezi kuyatekeleza haya tunayopanga pasipo kumshirikisha Mungu