More details

JIKINGE, TUISHINDE EBOLA

JIKINGE, TUISHINDE EBOLA Ugonjwa wa Ebola unaambukizwa kwa kugusa nguo za Mgojwa wa Ebola, kugusa maji maji ya mwili kama damu, mate, kinyesi, matapishi, kamasi, mkojo na na damu toka kwa Mgonjwa, kuchangia vitu vyenye ncha kali, kugusa wanyama pori walio hai au mizoga Dalili za Ugonjwa wa Ebola ni pamoja na homa Kali, kuumwa kichwa na vidonda kooni, mwili kuchoka, maumivu ya viungo,vipele, kutapika, kuhara, kutokwa na damu sehemu za wazi. Daliliza Ebola huanza kujitokeza kuanzia siku mbili hadi siku 21 baada ya kupata maambukizi. JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA EBOLA (i) Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au tumia vitakasa mikono. (ii) Epuka kugusa majimaji ya mwili, nguo, shuka, godoro, au vitu vingine vya mgonjwa mwenye dalili za Ebola. (iii) Epuka kugusa wanyama pori wakiwa hai au mizoga (iv) Epuka kula nyama ambayo haijapikwa vizuri, nyama mbichi au mizoga. Ukihisi Magonjwa ya dalili za Ebola, wahi kituo cha huduma ya Afya Vilevile toa taarifa kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa, kijiji au Kata uonapo mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Ebola. Kwa taarifa, Elimu na Ushauri piga simu namba199 bure Imetolewa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa Ufadhili wa UNICEF