More details

Jikinge, Tuishinde EBOLA

Tunapoelekea kwenye maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa nchi yetu ya Tanzania (9 Disemba 2022), tunakumbuka tangu mwanzo imekuwa ni kupambana na Ujinga, Umaskini na Maradhi. Na katika miaka yote hii Serikali yetu imejitahidi sana kuhakikisha ama tunapunguza ama tunatokomeza kabisa maadui hawa. Ebola ni moja ya maradhi sawasawa na COVID-19 ambayo tumeendelea kuwa nayo na sasa tunajielimisha mahali hapa kuona ni kwa namna gani tunaweza tukajikinga na maradhi haya. Kwa hiyo ni rai yangu kwa watanzania wote kuendelea kushirikiana na kufuata maelezo ambayo Wizara ya Afya pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatupatia sisi wananchi wake tuweze kushirikiana kwa pamoja. Mungu ametupatia miili ili tuweze kuitunza, na njia mojawapo ambayo tunatakiwa kuitunza miili yetu ni kuhakikisha kwa namna gani tunajikinga dhidi ya maradhi.