Tumewafikia viongozi wa dini 422 katika kuwapa elimu ya kujikinga na Ebola
Tumewafikia viongozi wa dini wapatao 422 katika kuwapa elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa Ebola. Viongozi hao wanatoka Mikoa ya Kigoma, Geita, Mwanza , Mara na Kagera. Kazi kuu ya viongozi hao ni kueleimisha waumini na jamii kwa ujumla juu ya kujikinga na janga hili kubwa la Ebola ambalo bado halijatufikia Tanzania. Tunachukua tahadhali kwa kuwa Uganda ni karibu na Mikoa hiyo.
Mkurugenzi wa Tanzania Interfaith Partnership-TIP Asina Shenduli wakati wa kongamano la maombi la viongozi wa dini mbalimbli jijini Mwanza.