More details

Kupinga ukatili wa Kijinsia kwa njia ya Burudani

Elimu ya Kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia kwa njia ya uimbaji imekuwa ikitumika na kuleta matokeo chanya katika maeneo mbalimbali mwa Tanzania. Hapa ni kikundi cha ngomba asili kikitumbuiza katika shule ya Sekondari Chamwino Jijini Dodoma. Ubakaji kwa watoto wa kike imekuwa ni moja ya changamoto inayowakabili watoto wa kike katika maeneo hayo. CCT imetoa elimu kwa wanafunzi hao na wazazi namna ya kulinda watoto hasa wa kike, moja ya mikakati ya kujiepusha na vitendo hivyo ni kutokutembe usiku na kutopita katika maeneo hatarishi kama vichaka