More details

Kongamano la ulinzi na Usalama wa mtoto mkoani Dodoma

CCT kupitia dawati la wanawake , maendeleo, jinsia na watoto imeendesha Kongamano la ulinzi na Usalama wa mtoto mkoani Dodoma katika viwanja vya nyerere square leo tar 20/Juni 2024. Katika Kongamano hilo Ndugu Urio Ndekirwa ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu CCT ameeleza kazi za CCT ikiwemo kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto. CCT katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia inashirikiana na BAKWATA, TEC, CPCT, SDA na wadau wengine kwa kuwa unyanyasaji wa kijinsia hauangalii dini. Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe Gift Msuya ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepongeza CCT kwa kuona umuhimu wa kuendesha kongamano hili ndani mwezi wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika. Amepongeza watoto kwa nyimbo mbalimbali zenye jumbe za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia. Mratibu wa dawati la maendeleo ya wanawake, watoto na jinsia Elizabeth Ngede ameomba kila mmoja kuenzi malezi bora kwa watoto. Amepongeza kamati ya dini mbalimbali Mkoa wa Dodoma kwa kusimamia vizuri zoezi hili la kumlinda mtoto kupitia tamasha hili. Swala la mlinzi na usalama wa mtoto ni swala endelevu na CCT itaendelea kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto ili kila mtoto aweze kukua katika maadili yanayoipendeza jamii.