More details

Kikao cha tathmini ya kazi za Viongozi wa dini mbalimbali Wilayani Simanjiro kwa mwaka 2024.

Viongozi wa kamati ya Dini Mbalimbali wilaya ya Simanjiro wamekutana leo katika kikao cha tathmini ya kazi mbalimbali zilizofanyika na kamati ya dini mbalimbali wilayani humo kwa mwaka 2024. Afisa programu wa mahusiano ya Dini mbalimbali –CCT Mch. David Kalinga ameipongeza kamati ya dini mbalimbali wilaya ya simanjiro kwa kazi kubwa walioifanya ndani ya wilaya hiyo ikiwemo kutatua migogoro katika jamii, kukemea vitendo vya ukatili, na kuhamasisha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.