More details

klabu za wanafunzi katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia

Semina ya mafunzo kwa klabu za wanafunzi katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji Kwa wilaya za Serengeti, Tarime na Rorya. Mafunzo haya yanatekelezwa katika wilaya ya Serengeti katika ukumbi wa kanisa la KKKT. Leongo ni kuwajengea uwezo watoto kukataa vitendo vya ukeketaji pia wao kuwa mabalozi katika kuelimisha watoto wengine. Kipindi ambapo shule zilifungwa kwa sababu ya Janga la Ugonjwa wa *COVID-19* , Watoto wengi hasa wa kike walikumbwa na changamoto ya kukeketwa na wengine kuozeshwa. Hali hiyo imekatisha ndoto za baadhi ya watoto wa kike katika maeneo yetu. Haya yamesemwa na wanafunzi walioshuhudia wenzao kukatisha masomo kutokana na matatizo hayo kutoka wilaya hizo. CCT kupitia idara ya Maendeleo na utetezi, Mama Askofu Muhagachi Mratibu Taifa wa Wanawake, Watoto na Jinsia ameendesha mafunzo kwa wanafunzi hao ili kuwajengea uwezo wa kuwa mabalozi wa kupinga vitendo vya ukatili hasa ukeketaji kwa watoto wa kike. Mafunzo yameambatana na elimu ya kujikinga na Ugonjwa wa *COVID-19* ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na kutumia vitakasa mikono. Mafunzo haya yamehudhuriwa na viongozi toka serikalini (idara ya elimu halmashauri ya Serengeti) na viongozi wa Dini toka makanisa wanachama CCT.