More details

Kamati ya viongozi wa Dini mbalimbali Mkoani Manyara

Viongozi wa kamati ya dini mbalimbali Mkoani Manyara wamekutana kujadili masuala ya haki, amani na demokrasia katika jamii yao inayowazunguka. Katika mjadala wao mojawapo ilikuwa ni kujadiliana namna ambavyo wananchi wanajua kazi za wabunge. Wengi wa washiriki wamesema wananchi hawajui kazi za wabunge isipokuwa wanajua wabunge kazi yao ni kuwakilisha wananchi bungeni. Hivyo wanakamati wamekubalianan kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wananchi ili wajue kazi za wabunge ni zipi ikiwa ni pamoja na kutunga sheria.