Kazi za ufuatiliaji wa mradi wa Tuwajibike

Kazi za ufuatiliaji wa mradi wa Tuwajibike zikiendelea katika Mikoa ambako mradi unatekelezwa (Kigoma(DC), Dodoma (Bahi), Shinyanga (Kishapu), Tabora(Nzega) na Pwani (Kibiti)).

Wanakamati wa MURU wanaeleza namna ambavyo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuhamasisha wanajamii kushiriki mikutano mbalimbali ya Kijiji, kufuatilia rasilimali za umma kukuza uwazi, uwajibikaji na kuhimiza wanachi kushiriki katika kupanga, kutekeleza, kusimamia na kufuatilia rasilimali za umma.

MURU ni Mfumo wa Ufuatiliaji wa Rasilimali za Umma unaojulikana kwa lugha ya Kiingereza kama Public Expenditure Tracking Systems or Surveys (PETS) ambao ni dhana ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma inayokuza uwazi, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika kupanga, kutekeleza, kusimamia na kufuatilia rasilimali za umma

Scroll to Top