Kikao ni cha tamthimini ya kazi zilizotekelezwa na viongozi wa dini kwa mwaka 2024

Viongozi wa Kamati ya Dini Mbalimbali Wilayani Kiteto na Simanjiro wakiongozwa na Mch. David Kalinga Afisa Programu wa mahusiano ya Dini Mbalimbali-CCT wamekutana na kufanya kikao kifupi na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe.Remidius Mwema (ofisini kwake) na Mkuu wa Wilaya Simanjiro Mhe.Fakii Raphael Lulandala(ofisini kwake) kama inavyoonekana katika picha. Kikao ni cha tamthimini ya kazi zilizotekelezwa na viongozi wa dini kwa mwaka 2024 ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji, Kupambana na Vitendo vya ukatili wa kijinsia, kuimarisha mahusiano mema kati ya dini zote , elimu ya kila mmoja kutambua wajibu wake n.k

Scroll to Top