CCT imetoa mafunzo ya ushauri nasaha kwa wakuu wa shule, walimu washauri kutoka shule zilizoko chini ya makanisa wanachama CCT kutoka Kanda ya Maashariki yenye Mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Zanzibar, Tanga na Morogoro.
Mafunzo yamefanyika kwa siku mbili ambapo siku ya kwanza mafunzio yalifanyika kwa walimu wakuu wa shule na Waratibu wa Elimu kutoka makanisa wanachama wa CCT wanaomiliki shule za sekondari na vyuo. Siku ya pili mafunzo yalifanyika kwa walimu kutoka makanisa wanachama wenye shule za Sekondari.

Mafunzo yamelenga walimu kujua namna nzuri na kusaidia kutoa ushauri katika taaluma na Ushauri nasaha kwa wanafunzi ili kulinda watoto katika tabia zao na kuwasaidia katika kufikia malengo yao kwa usahihi. Ikumbukwe tusipowalea watoto katika maadili mema watapotenza ndoto zao.
Mambo ambayo wamesisitizwa wakati wa kutoa ushauri nasaha kwa mtu mmoja mmoja ni pamoja na
a. Kumsikiliza unayempatia ushauri wa kitaaluma na ushauri nasaha.
b. kumhakikishia usiri wa mazungumzo.
c. kumpa nafasi ya kujieleza kwa uhuru,
d. kumjengea mazingira ya kumtoa katika tatizo alilo nalo.
e. mwalimu usiwe mtoa majibu, bali atapaswa kuwa msikilizaji mzuri. Mwalimu kuwa na uelewa wa kutosha katika kutoa ushauri wa kitaaluma pamoja na ushauri nasaha.

f. Mwalimu kujiamini katika kutoa ushauri, kumjengea mwanafunzi(mteja) uhuru wa kujieleza.
Mafunzo yamefungwa na Baba Askofu Philipo Mafuja wa Afrika Inland Church Dayosisi ya Pwani ambapo amepongeza zoezi zima la uratibu wa mafunzo hayo na amewashukuru walimu ambao wameweza kushiriki mafunzo haya ya kuwasaidia wanafunzi shuleni/vyuni katika kukabilianana tabia mbovu, utandawazi na changamoto za ajira .
Walimu tusiwalazimishe watoto kuchagua masomo, bali tuwasikilize mapendekezo yao na kuwasaidia/kuwashauri kupitia mapendekezo yao. Watoto tukiwalea vizuri kanisa litakuwa limewekeza vyakutosha, amesema Baba Askofu.

Hata katika maandiko tunaonyeshwa Yoshua wakati anaongoza wana wa Isarael aliwaambia wachague ni nani watakayemtumikia(Guidance). Yesu aliwaelekeza (guide) wanafunzi wake (Mathay 7 :13-14) habari ya njia ya kwenda mbinguni, akisema kuna njia nyembana na pana, pale alikuwa anawashauri.
Tunatamani wanafunzi wawe wacha Mungu kwa kuwafanya wawe watiifu, watimize kusudi la Mungu, wawe na tabia ya amani, kuishi nuruni(kuwa nuru katika jamii) na kulishika neon la Mungu.