More details

Matokeo ya mradi wa mwanamke Jasiri kwa Dada Eda paul

Katibu mkuu CCT Mchg Canon Moses Matonya akishuhudia matokeo ya mradi wa mwanamke Jasiri kwa Dada Eda paul ambaye ni mwanakikundi wa kikundi cha Amani toka Wilaya ya Kongwa Dodoma. Alianzisha duka la kushona nguo ambapo alianza na cherehani moja,baada ya kupata mafunzo ya ujasiliamali aliamua kuongeza cherehani mbili zikawa tatu. Alifanikiwa kuanzisha mafunzo kwa wanafunzi wengine ambapo alianza kupokea wanafunzi ambao anawafundisha kwa kipindi cha miezi sita. Kupitia mafunzo ya mradi ameweza kuongeza kipato chake na kupanua mradi hivyo ameanza na kuuza nguo za aina mbalimbali katika kibanda hicho. CcT kupitia Mradi wa mwanamke Jasiri unaofadhiriwa na NORAD imekuwa ikiwajengea uwezo wanawake katika kupanua miradi yao ikiwa ni pamoja na kuhimiza wajasiriamali hao kuajiri vibarua na kubuni miradi mipya kwa ajili ya kukuza miradi itakayowaongenea kipato. Kikundi cha Amani ni moja ya vikundi ambavyo vimenufaika kwa kiwango kikubwa kutokana na mafunzo yanayotolewa na matokeo yao yanaonekana.