More details

Kikundi kimefanikiwa kuvuna magunia 37 ya mpunga

Picha ni kikundi cha Tupendane toka kijiji cha Urunda Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya wakati wa mavuno ya mpunga kwa kutumia mashine iitwayo Combine Harvester _ambayo wamekodi kwa ajili ya kurahisisha kazi hiyo. Mbinu za kilimo cha kitaalamu zimetiwa chachu na mafunzo ya mradi wa mwanamke jasiri ambao umekuwa ukitoa mafunzo ya kuimarisha shughuli za uzalishaji kwa vikundi vya wanawake wajasiriamali. Kikundi kimefanikiwa kuvuna magunia 37 ya mpunga eneo la ekari moja walilolima zao hilo. Mratibu wa mradi wa mwanamke Jasiri Mkoa wa Mbeya Faustina Godwin amekitaja kama kikundi cha mfano katika kutekeleza yale ambayo walifundishwa na wataalamu wa kilimo kupitia mradi wa mwanamke Jasiri kwani awali kabla ya mafunzo mavuno yalikuwa kidogo ambapo kwa ekari moja walikuwa wanapata wastani wa gunia 15. Mradi wa mwanamke jasiri unasimamiwa na CCT kwa ufadhiri wa Shirika la maendeo la Norway(NORAD)