More details

CCT yabuni mbinu ya Kutatua Changamoto za Biashara kwa Wajasiriamali wadogowadogo

CCT yabuni mbinu ya Kutatua Changamoto za Biashara kwa Wajasiriamali wadogowadogo* Baadhi ya changamoto zinazowakabili wajasiriamali wadogowadogo (wanavikundi) ni kukosa vifungashio kwa bei ya chini kitu ambacho kinawafanya wauze bidhaa zao kwa bei ya juu hivyo kukosa wateja. Ukosefu wa eneo maalumu la kujenga viwanda vya wajasiliamali wadogowadogo nalo ni changamoto kiasi kinachowafanya waendeshe shughuli zao majumbani ambapo sio sehemu sahihi, mfano utengenezaji wa bidhaa za kemikali kama sabuni. Pia ukosefu wa elimu ya ujasiliamali ni changamoto inayowafanya waendeshe kazi zao kwa njia zisizo za kibunifu. Afisa Biashara H/Jiji la Dodoma Bi Donatha Vedasto na Afisa Maendeleo katika Jiji hilo Bi Hidaya Mizega wameungana na maombi ya wajasiriamali hao kwa kuwahakikishia mpango mzuri wa kuwatengea eneo rasmi kwa viwanda vya wajasiliamali wadogowadogo. CCT kupitia Mradi wa mwanamke Jasiri imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali yanayolenga kuinua uchumi wa jamii kupitia wanavikundi, ambapo leo imetumia mbinu ya kuwawezesha viongozi mbalimbali toka Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kutoa elimu ya kukabiliana changamoto zinazowakabili wajasiliamali wadogowadogo na kutoa njia sahihi za kukabiliana na changamoto hizo. Mafunzo haya yametolewa kwa viongozi(wawakilishi) wa vikundi vya mtandao(Kilimo, ufugaji, upambaji, kuweka na kukopa, usindikaji,ushonaji, n.k) vinavyosimamiwa na mradi huo Mkoa wa dodoma. Mafunzo haya yamehudhuriwa na watumishi toka CCT chini ya Mradi huo ambao ni Mkurugenzi wa Programu za Maendeleo na Utetezi Bi Clotilda Ndezi, Afisa Mradi (Uchumi) Bw.Azgard Stephen, Afisa tathmin na Ufuatiliaji Bw Urio Ndekirwa Gabriel, Mratibu wa mradi Bi Christina Motto, Mratibu wa mradi Mkoa wa Dodoma Elizabeth Ngede na watumishi wengine.