More details

Wanavikundi wanajenga Jengo lenye ukumbi mkumbwa wa Biashara

Serengeti Wanavikundi wanajenga Jengo lenye ukumbi mkumbwa wa Biashara Tumeungana vikundi saba vya VICOBA tukiwa jumla wanachama 170, na tunajenga jengo lenye ukumbi kwa ajili ya mikutano yetu na kwa ajili ya biashara kama mikutano na sherehe mbalimbali. Jengo hilo lina vyumba vitatu vya kibiashara kwa mbele ambavyo tutaweka wapangaji. Jengo letu kwa ndani lina vyumba vitatu kwa matumizi ya kutunzia kumbukumbu za VICOBA. Tunatarajia kufanya harambee tarehe 26/Feb 2021 ili kupata fedha za kupaua jengo. Hatujaanda mgeni rasmi, tutafanya tukio hilo sisi wenyewe wanavikundi. Ni Marwa Nyantori Mhudumu wa kujitolea (Volunteer) chini ya CCT kata ya Rungabure Wilaya ya Serengeti wakati akitoa mrejesho wa kazi zilizofanyika mwaka 2020.