Baba Ask Shoo ongoza Ibada ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Jengo la Kitega Uchumi CCT Tar 2 Disemba 2024
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania Mhashamu Baba Askofu Dkt.Fredrick Shoo ,ameongoza Ibada ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Jengo la Kitega Uchumi (CCT Commercial Complex). Jengo hilo linajengwa linajengwa jijini Dodoma mkabala na ofisi za CCT Makao Makuu.
Jengo hili ni alama ya kuendelea kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na viongozi waasisi wa CCT. Dkt. Shoo amesema.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa CCT Mch.Dkt. Canon Moses Matonya amesema Jengo hilo litakapokamilika litasaidia kuongeza mapato ya CCT, hivyo kuongeza ufanisi na utekelezaji wa kazi mbalimbali za Taasisi ikiwemo Uinjilisti na Uratibibishaji wa Elimu ya Kikristo Mashuleni.
Ibada hii imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa CCT ,Watumishi wa CCT na baadhi ya Viongozi wa mashirika wanaofanya kazi pamoja na CCT.