Mhe. Doto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amefungua Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania-CCT leo hii katika Ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma.

Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Makanisa 12 wanachama wa CCT na vyama vishiriki 14 vya kimisioni vya CCT.
Siku ya pili umefanyika katika Ukumbi wa CCT Commercial Complex jijini Dodoma. Mkutano huu umeambatana na uchaguzi Mkuu Wa Viongozi Wa Jumuiya hiyo.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Makanisa 12 wanachama wa CCT na vyama vishiriki 14 vya vishiriki vya CCT.

MATOKEO YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAPYA WA JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA (CCT) 2025 – 2029
1. Askofu Dkt. Stanley Hotay – Mwenyekiti
2. Askofu Dkt. Abednego Keshomshahara – Makamu Mwenyekiti wa Kwanza
3. Askofu Nelson Kisare – Makamu Mwenyekiti wa Pili
