More details

Elimu kwa vitendo namna ya kutengeneza chakula cha ziada

Afisa kilimo,mifugo,uvuvi na ujasiriamali wa CCT kupitia mradi wa lishe endelevu, Sembael Mfangavo akitoa elimu kwa vitendo namna ya kutengeneza chakula cha ziada(uji wa lishe) kwa watoto kuanzia umri wa miezi sita na kwa kina mama wajawazito na wanaonyonyesha. Mafunzo haya yamefanyika katika kikundi cha Tupendane kilichopo kata ya kikuyu kaskazini mtaa wa mission wilaya ya Dodoma jiji. Aidha ikiwa lishe ni swala mtambuka Afisa huyo amepata wasaa wa kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima wa mbogamboga namna ya kutambua wadudu na magonjwa shambulizi na njia sahihi ya kukabiliana nayo katika bustani za mbogamboga wanazolima ikiwa ni sehemu ya upatikanaji wa mlo kamili. Kikundi hiki kinasimamiwa na CCT kupitia mradi wa lishe endelevu unaofadhiliwa na USAID. Tupendane ni kikundi ambacho kimeshatembelewa na Katibu Mkuu wa CCT Mchg.Canon Dkt.Moses Matonya kuona shughuli wanazotekeleza. Lishe Endelevu imekuwa ikitoa elimu ya lishe kwa jamii hasa kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, vijana erika balehe na wanaume ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa watoto walio katika umri chini ya miaka miwili na upungufu wa damu kwa kina mama wajawazito. Jamii inafundishwa kujikita katika uzalishaji na ulaji wa mazao ya mbogamboga kwa lengo la uimarisha afya. Kupitia mradi huu CCT imeweza kufikisha elimu hiyo kwa wilaya nne za mkoa wa Dodoma zikiwa ni Dodoma jiji,Halmashauri ya Bahi,Kondoa TC&DC