More details

Mission & Evangelism

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania-CCT Askofu.Dkt.Fredrick Shoo pamoja na Katibu Mkuu wa CCT Mch.Canon.Dkt. Moses Matonya wameshiriki Maombi ya dunia Kitaifa Mkoani Tabora,maombi hayo yameratibiwa na Idara ya Maendeleo ya Wanawake,Watoto na Jinsia -CCT kwa kushirikiana na kamati ya Wanawake CCT Mkoa wa Tabora. Katika maombi hayo Mwenyekiti wa CCT amewapongeza CCT Mkoa wa Tabora kwa maandalizi mazuri ya maombi ya dunia,pia amewasisitiza wanawake kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu. Katika hatua nyingine Mhe. Deusdedith Katwale Mkuu wa wilaya ya Tabora amewapongeza wanawake wa CCT kwa kuandaa maombi hayo na kusema serikali inaendelea kufanya kazi kukomesha vitendo vya ukatili zidi ya wanawake kwa kutunga sera,sheria na kanuni mbalimbali zitakazosaidia kukabiliana na vitendo vya ukatili. Wanawake zaidi ya 1800 kutoka makanisa mbalimbali ya CCT ndani na nje ya Mkoa wa Tabora wameweza kushiriki maombi ya dunia kitaifa.